MECHI YA SIMBA NA YANGA ILIINGIZA SH. 260,910,000.

0

41,733 WASHUHUDIA MECHI YA SIMBA, YANGA

*Watazamaji 41,733 walikata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga iliyochezwa jana (Mei 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.** **Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 VIP C, sh. 30,000 VIP B na sh. 40,000 VIP A. Watazamaji 36,980 walinunua tiketi za sh. 5,000 wakati 203 walikata za sh. 40,000.** **Mechi hiyo ambayo ni moja kati ya saba zilizochezwa siku hiyo kufunga msimu wa 2011/2012 iliingiza sh. 260,910,000.

0 comments: