MFAHAMU MWANAMUZIKI WA KIKE TAJIRI ZAIDI DUNIANI N A UTAJIRI WAKE.
0
Ukitaja wakongwe na magwiji wa muziki duniani hutasahau au kumuacha mwanamama huyu ambaye ana kila aina ya sifa kwenye swala zima la uimbaji na huyo si mwingine bali ni Madonna Louise Ciccone ambaye pia ni mtunzi wa nyimbo,mwigizaji na mfanya biashara. Mwanamama huyo anamilii utajiri wa dola za Kimarekani milioni 650 alioupata kutokana na show,kuuza kazi zake na kucheza filamu na ameuza zaidi ya nakala milioni 300. Anamiliki nyumba 10 kwenye nchi za Uingereza na
Marekani,anamiliki gari la bei mbaya kuliko yote Maybach
linalouzwa dola za kimarekani milioni 524 na magari mengine kama BMW na Range, anamiliki ndege aina ya Gulf Stream kwa ajiri ya safari zake binafsi, Madonna alianza mambo ya muziki mwaka 1977 na alianza kama dansa kwenye makundi ya Breakfast Club na Emmy.