MJUE TAJIRI MKUBWA DUNIANI ANAYEISHI NA PAPA NYUMBANI KWAKE!!

0


Huyu ndiyeyule mwanzilishi na mmiliki wa Microsoft ambayo inahusika na utengenezaji pamoja na usambazaji wa Program za kompyuta, Jina lake harisi likiwa Willium Henry maarufu kama Bill Gate ambaye ni tajiri namba mbili duniani baada ya Carlos Slim raia wa Mexico, Bill ana utajiri wa Dola 61.3 bilioni. Ana nyumba eneo la Medina jijini Washngton yenye thamani ya dola 125 milioni ambayo imepakana na ziwa Washngton huku James Cutler akiwa mbunifu wa nyumba hiyo kwa kutumia kompyuta na aliijenga kwa kupasua mlima ulio karibu na ziwa hilo. Chini ya nyumba hiyo kuna bwawa la samaki ambalo lina samaki mbalimabali
wakiwemo papa ambao huonekana wakipita chini ya nyumba hiyo kwani
sakafu yake imejengwa kwa vioo pamoja na kuta zake ambavyo vinahimili uzito mkubwa, Pia anamiliki magari kama Porsche 959 coupe,Lincolin continental,Ford Focus na Limousine Chevrolet Corvette, pia nanamiliki ndege nne ikiwemo ile Bombardier BD-700 Global Express yenye thamani ya dola 45.5 milioni na pia anamilki boti ghali sana duniani ya Goygpus!.


0 comments: