KESI YA ELIZABETH MICHAEL_LULU YASIKILIZWA LEO NA UTATA WAIUBIKA!!
0
Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam Bi. Augustina Mmbando mapema leo msanii wa filamu Tanzania ambaye anahusishwa na kifo cha msanii mwenzake pia wa filamu Steven Kanumba amesimama kizimbani akikabiliwa na shtaka hilo huku mahakama ikiamuru mtuhumiwa huyo kutojibu lolote kuhusiana na kesi hiyo.Utata uliibuka wakati Mawakili wanao mtetea Lulu Keneth Fungamtama, Fulgence Massawe, Peter Kibatala na Jackline De Meero, Ambapo
Wakili Fungamtama alidai Mahakamani hapo kwamba kutokana na umri mdogo wa mtuhumiwa wanaiomba Mahakama itoe udhuru kwa mtuhumiwa Elizabeth kushitakiwa katika Mahakama ya watoto kwa kuwa ana umri chini ya miaka 18 pia kesi yake iwe INCAMERA ombi ambalo lilitupiliwa mbali na mahakama hiyo kwa kutumia kifungu cha sheria namba 196 kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za jinai hivyo ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 21 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena. Hivyo Lulu amerudishwa Segerea hadi kesi yake itakapotajwa tena!.