Jacqline ameandika kwenye blog
yake na namkariri akisema “kiukweli mimi kama Jacquline Wolper sina
ubaya na mtu yeyote, ila nmeshangaa kuona watu nisiyo wajua kuja usiku
wa manane na kunichomea gari yangu. Kiukweli siwezi kumuhisi mtu ila
najua ni lazima atakua mtu asiependa maendeleo yangu ni ni mtu mbaya
sana kwangu. Na inawezekana kabisa alipanga kunia lakni kwa bahati nzuri
siku hiyo sikua nyumbani nilikua nimesafiri. Tukio lilitokea usiku wa
tarehe 23/10/2012 ambapo mtu alitumia matambara yaliyo na mafuta ya taa
au Petrol akiwa kwa nje ya ukuta wa nyumba yangu akiwa anarusha kwa
ndani. Nimepeleka taarifa kituo cha Polisi kawe kwa kutaka msaada wa
kiupelezi na nitakua nawapa taarifa za kila kinachoendelea. Namshukuru
Mwenyezi Mungu kwani niko salama” |