HIVI NDIVYO RICHY ONE ALIVYOTEGWA MPAKA KUSWEKWA LUPANGO KWA TUHUMA ZA KUMHUJUMU ALI KIBA

0

 

Richy One akiandikisha maelezo kituoni
Jumatatu iliyopita kulikua na Breaking News kwenye Kipindi cha XXL ya Clouds fm, kwamba Msanii wa Bongo flava Richy One amekamatwa na kupelekwa polisi kwa tuhuma za kufanya udanganyifu kwa ku divert namba ya simu ya Ali Kiba hivyo simu zote alizokua anapigiwa Ali Kiba zikawa zinaingia kwenye simu ya Rich One, hapo maana yake Deal/michongo yote ya Ali Kiba kuanzia madeni na Bookings za show za Ali Kiba zilikua zinaingia kwenye simu ya Richy One (Inasemekana lakini)
Kwa mujibu wa Mdogo wake Ali Kiba anaitwa Abdu Kiba (nae ni msanii wa muziki wa kizazi Kipya) anasema baada ya kaka yake yake kumwambia kuwa design namba yake kuna mtu ameichakachukua, ndipo Abdu akaamua kutumia ujanja wa kumpigia huyo mtu Ali Kiba Feki, akamwambia Laki tano yako nakupatia vipi? wapi nikuletee? Ali Kiba Feki udenda ukamtoka/ akautamani mkwanja, mwisho wa siku wakapanga wakutane Postaaa kesho yake asubuhi, Ally Kiba feki akadai kuwa yuko busy na kikao hivyo atamwagiza kijana wake aje kuchukua mkwanja huo Kwa Abdu Kiba, akampa na  namba za kijana wake, asubuhi yake Kijana akawa anawasiliana na Abdu Kiba, Heee lahaula Kuja kutahamaki Abdu Kiba anamwona Richy One ndo anajitambulisha kama yeye ndio Kijana aliyetumwa na Ali Kiba feki kuja kuchukua mpunga/ Laki 5, Abdu Kiba alikua ameongozana na vijana wengine, basi wakamkamata na kumpeleka Richy One polisi Msimbazi Kariakoo, akahojiwa na kuachiwa baadae kwa dhamana.
Na inasemekana mpaka leo Ali Kiba feki(bosi wake Richy One) bado hajapatikana

0 comments: