wale wa gosip...cheki hii ki2
0
Mbunge wa Jimbo la Kawe, kupitia Chama cha CHADEMA, Halima Mdee (kulia) akigoma kuangalia keki ya Birthday ya Mbunge wa Bunge la Afrika... Mashariki kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Shy-Rose Bhanji, na kugeuka pembeni akidai anaathiriwa na rangi ya keki hiyo wakati wa sherehe fupi ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Mbunge Shy-Rose, iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Picha kwa hisani ya mrokim.blogspot.com
**************************************
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi waliangua Vicheko pale wenzao wa CHAMADA walipoikwepa kuigusa nakuila Keki ya Birthday ya Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Shy Rose Banji wakati wa tafrija yake iliyofanyika Nyumbani Longe Jijini Dar es Salaam.
Wabunge hao wa CHADEMA ni Halima Mdee (Kawe) ambaye anaonekana picha ya juu akiikataa keki hiyo iliyotolewa na Wakurugenzi wa Nyumbani Longe, Gadna G Habash na Mkewe Lady Jay Dee, huku Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Kiwelu picha ya chini nae akijificha asiitazame kwa karibu.
Wabunge hao waliigwaya Keki hiyo kutokana na jinsi ilivyopambwa rangi za CCM.
Huku Wabunge wa CCM wakishangilia wakimtaka Halima Mdee aongoze Ukataji wa Keki hiyo ambayo ilitolewa baada ya keki ya awali iliyoandaliwa na Baby Girl Shy Rose kuliwa, ilishindikana kuliwa na kuhifadhiwa.
Watu mbalimbali walihudhuria tafrija hiyo ndogo wakiwepo Wabunge, wanasiasa, Wasanii musiki, Watangazaji na Wanahabari ambapo kila aliye simama kuongea alimpongeza sana Shy Rose kwa kuwa Mpambanaji wa Ukweli katika kutafuta kile anachotaka na kumuombea kwa Mungu amuongoze vyema katika kazi yake.