KARABANI: NAIPENDA NCHI YANGU THATS WHY SIONI HAJA YA KUKWEPA MABANGO KWENYE VIDEO ZANGU

0



Karabani
Director wa Music Videoz Maarufu kama Karabani amefunguka sababu ya Touch zake kuonyesha mabango ya matangazo mbalimbali ni kutokana na Tanzania hakuna sheria ya nzuri zinazo elekeza kampuni za matangazo wapi pa kuweka bango wapi wasiweke, kutokana na hilo mabango na Posters zimekua zikiwekwa hata sehem sizizo rasmi, kitu ambacho watu kama yeye wakiwa wanashoot film inakua ngumu kuyakwepa kwani zaidi yeye hupenda kuonyesha uhalisia wa sehem husika.
Karabani akaendelea kufunguka kuwa yeye anaipenda sana Tanzania thats anapenda kushow case uhalisia wa Bongo ulivyo. namnukuu "mbona hata video ya B.I.G ...More Money More Problem wamei shoot New york City na ina matangazo kibao ndani yake"
Karabani alifunguka hivi karibuni katika Kipindi cha XXL ya Clouds Fm, baada ya msikilizaji mmoja (Mtoto wa Vitoto) kutuma Email inayosema kuwa Video za Karabani zina mabango mengi ndio maana hazipati nafasi ya kuchezwa kwenye TV station za kimataifa.
Kuhusu Videos kutoonyeshwa kimataifa, Karabani amejibu si kweli, kwani project zake nyingi ziko worldwide

0 comments: