ASHANTI AFANYIWA MAHOJIANO NA MAMA YAKE KATIKA KUIPA HESHIMA SIKU YA MAMA DUNIANI.

0


Mshindi wa tuzo ya Grammy, Ashanti alikaa na mama yake kwenye mahojiano ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya mama duniani. Alikuwepo mama yake pamoja na meneja wake Tina Douglas katika mahojiano ndani ya AOL Music. Katika mahojiano this time ilikua tofauti, Tina meneja wake ndo alikua anamuuliza maswali, Alimuuliza juu ya ushauri mzuri anaompatia na akamuuliza kumuelezea mwanamke katika famila yake, Hata dada Shia alijiunga. “ Kila wakati ulinifundisha kuwa kiongozi sio mfuatajifuataji tu, niwe na maamuzi yangu” Alisema Ashanti ambaye album yake ya “BraveHeart” inatoka Juni. “ Kwa wepesi kila wakati ushauri huo nimeufuata mpaka na nashukuru sana kwa ushauri huo” Aliongeza.

0 comments: