KAULI YA WEUSI KUHUSU KUKAMATWA KWA LORD EYES.

0

.
Msemaji wa kundi la Weusi Nikki wa Pili ametoa kauli ya kwanza toka kukamatwa kwa Lord Eyez wa kundi hilo kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya gari la Ommy Dimpoz.
Namkariri Nikki wa Pili akisema “kwanza hiyo ni habari ya ghafla alafu ni ya kusikitisha na kushtua, ni habari ambayo imetupa shida na mpaka sasa inatupa shida sana kwa sababu watu wengi wanatupigia simu kutuuliza inakuaje”
“Ukiangalia kwenye mitandao ya facebook na twitter kote imesambaa, unajua ukijua ukweli ni kitu cha msingi sana kwa sababu sisi pia tulikua hatufahamu kilichotokea, kwa hiyo cha kwanza tulichokifanya ni kutaka kujua kilichotokea, mfano mimi niliona kwenye mitandao kwamba Lord Eyes amekamatwa kwenye eneo la tukio yupo kwenye gari lakini kufatilia nikaja kugundua haikua eneo la tukio na sio gari hilo,  uhalifu ulifanyika alhamis na alikamatwa jumamosi” – Nikki wa Pili
“Kitu cha busara tulichoamua kufanya tumeamua kufatilia kisheria ili tujue uhalisia ni upi ili tuweze kutoa tamko kwa sababu sisi wenyewe Lord Eyez hatujamuona wala hatujaongea nae, na kingine ambacho kinasikitisha ni kwamba Lord Eyez ndio ametuhumiwa kama mtu binafsi lakini ukiangalia kwenye mitandao watu wanawashambulia weusi kitu ambacho sio sahihi kabisa, mimi Joh Makini, Bonta, G Nako tumepokea hiyo habari kama mtu mwingine yeyote” – Nikki wa Pili.
.
.

0 comments: