EXCLUSIVE: ALICHOSEMA MATONYA KUHUSU STORI ZA MAENDELEO YAKE KUVURUGWA NA USHIRIKINA.

0

.
Kwa yeyote anaefatilia bongofleva toka kitambo kidogo najua jina la Matonya lazima litakua kwenye list ya familia ya wanabongofleva.
Ni jina ambalo limekua kwenye vichwa vya vizito vya habari mara kadhaa kutokana na stori kama ya kukamatwa na dawa za kulevya Chinapamoja na stori nyingine.
Stori ya mwisho mimi kuisikia na nikawa na hamu ya kuifahamu ni kuhusu taarifa kwamba msanii huyu mzaliwa wa Tanga 96.0 amekwama kwenye ishu zake za maendeleo kwa sababu kuna watu wanamloga asifanikiwe tena ikiwemo kukwamisha uzinduzi wa hoteli yake aliyoijenga Tanga ambayo ilitakiwa kufunguliwa toka miezi sita iliyopita.
Namkariri akisema “nilikua na harakati hizo za kufungua hoteli lakini majukumu yalinizidi nguvu kidogo lakini taratibu yangu iko palepale japo ile time niliyotarajia haikufanikiwa lakini bado nina mpango huo japo sitotaja siku, kuhusu ushirikina hiyo inasemekana lakini siwezi kusema ni kweli au sio kweli kwa sababu hayo ni mazingira ambayo yametuzunguka, mazingira yetu sisi waswahili”
“Siwezi kusemea swala hilo liko vipi lakini kikubwa tunapigana kila siku sichoki kumuomba Mungu kwa sababu siku zote penye mazuri hakukosi kuwa na mabaya kwa hiyo yanayosemwa labda ni ya kweli au sio kweli” – Matonya
Hoteli yake ni ya vyumba 10 ambapo ina pub ndani yake.

0 comments: