ULISIKIA ALICHOSEMA KALAPINA KUHUSU PROFESA J, ROMA, FID Q, LUNDUNO, RADO NA WENGINE? KIKO HAPA.

0

Kalapina.
Msanii wa hiphop Kalapina wa kikosi cha Mizinga amekubali kutaja majina ya wasanii wa hiphop anaosikiliza muziki wao kwa sasa hapa Tanzania.
Namkariri akisema “Tanzania mimi nasikiliza wasanii wote niangalie vitu wanavyovifanya lakini wasanii wengi hawako real wanafake, sasa hivi nimekua nikiwasikiliza wadogo zangu Lunduno, Nash Mc, Fid Q, Mansu Lee, Rado… mzee mwenzangu Profesa J amepotea sasa hivi, nilikua namsikiliza lakini sasa hivi amepotea”
“Profesa J amefikia hatua anafanya video za dada zetu wako uchi kabisa na ule ni udhalilishaji wa kijinsia kama atabisha si udhalilishaji, achukue video awachukue dada zake na mama zake wadogo awavalishe vichupi na sidiria tutaona kweli yeye ni mmagharibi lakini kama anachukua dada za watu huu ni udhalilishaji wa kijinsia mi napinga mambo kama yale, tusifikie huko sasa hivi huwezi kufanya video kali mpaka uweke wanawake wako uchi Tanzania” – Kalapina
Kalapina alipoulizwa kama ameshawahi kuongea na Profesa J kuhusu hilo amejibu “Prof sijabahatika kukutana nae kwa karibu lakini najua ujumbe huu utamfikia kwa sababu yeye ni mtu mzima na haya maneno ni mazito na sio kwa uadui, kwa ajili ya kujenga Profesa jina kubwa kabisa ni mtu ambae ana hadhi kubwa kwenye game hii hapa lakini namkumbusha, binadamu sometimes tunajikwaa tunapotea, namkumbusha kwa kweli sijapendezwa na video zile madada wako uchi kabisa chupi na sidiria, ule ni udhalilishaji wa kijinsia alafu hawa wanaharakati wa kutetea haki za wanawake siwasikii kupigia kelele maswala haya”
Kwenye line nyingine Kalapina amesema “nyimbo zangu zote nimekua nikizungumza haki za binadamu natetea wanyonge na ndio maana nimekua naonekana mtu tofauti na watu wengine sipewi ile support ya kutosha leo hii Wafalme wa hiphop wanaitwa akina Roma, hawa ni vijana wadogo zangu sana tungo zao kama unataka kuzilinganisha na zangu ni sawa sawa mwanafunzi wa nusery school umlinganishe na mwanafunzi wa chuo kikuu”

0 comments: