BAADA YA Z ANTO KUACHANA NA HUYU BINTI, ASEMA YUKO TAYARI KUOA TENA.
0
Wote tunafahamu kwamba Z Anto star wa hits kama Binti Kiziwi na Mpenzi Jini, alioa akiwa na umri wa miaka 22 tu tena siku chache baada ya video ya Binti kiziwi ilipotoka ambapo alimuoa mrembo alieuza kwenye hiyo video.
Walikaa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda wa mwaka mmoja na kuoana kwenye ndoa ambayo haikumaliza mwaka mmoja, ilivunjika Miaka mitatu iliyopita.
Z Anto anasema “niliamua kumuoa kwa sababu pesa ninazo mali ninazo na nikawa sipendi kuendelea kutenda dhambi, lakini tuliachana kwa sababu ya tamaa zake za kibinaadamu”
Huyu ndio mrembo alieonekana kwenye video ya Binti Kiziwi ambae ndio Z Anto alimuoa na wakaachana baadae.