MANCHESTER CITY WAWEKA HISTORIA MPYA ENGLAND,FERGUSON HOI!!

0


QPR walikokuwa wakicheza pungufu uwanjani wameipa mwanya Man city kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England baada ya kuwa na kiu nao toka mwaka 1968, Dakika ya 48 Joey Barton alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Carlos Tevez hivyo kuipa City nafasi kubwa ya ushindi. Goli la kwanza la City liliwekwa kimiani na Pablo Zabaleta kunako dakika ya 39 lakini Djibril Cisse aliisawazishia QPR dakika ya 48 huku goli la pili la QPR likifungwa na Jamie Mackie na kuifanya
City kuhaha
uwanja mzima kutafuta magoli, Lakini bila ya kutarajia kunako dakika za majeruhi Edin Dzeko akasawazisha dakika ya 90 na Sergio Aguero akapiga la ushindi dakika ya sekunde chache baadaye.

0 comments: