LINEX AMTANGAZA MKE WAKE MTARAJIWA

0
Staa wa single za Mama Halima, Moyo wa Subira na nyingine kadhaa, mwimbaji Linex mwenye umri wa miaka 28, ametangaza ndoa yake ambayo Mungu akijalia ataifunga november mwaka huu na mtasha wake raia wa Finland aitwae Suvi. Linex amesema japo mpenzi wake yuko kwao kwa sasa bado mapenzi yao yako strong huku mwaka mmoja ukiwa umepita tayari toka wameanza kuwa pamoja ambapo walikutana kwenye ndege wakati wakitoka Nairobi na Suvi ndio alikua anakuja Tanzania kwa mara ya kwanza. Kilichowafanya hasa waanze mazungumzo ni pale mrembo huyo alipohitaji msaada wa ramani ya alikokua anafikia ndipo Linex akaulizwa, bila tatizo akampa maelekezo ya kutosha ambapo hata walipotua ilibidi Linex na mshkaji wake wampeleke sehemu aliyohitajika kufikia. Baada ya hapo Linex alimwachia namba yake ya simu na wakaanza kuwasiliana ambapo kabla ya kuingia kwenye mapenzi walikaa kwenye urafiki wa kawaida kwa kama miezi minne. MSIKILIZE LINEX HAPO CHINI:

0 comments: