ULAYA HAWANA MDA WA KUPIGA WEZI WAO,WANAWAADABISHA KWA MTINDO HUU

0




SHILOLE AFUNGUKA KUHUSU VIFO VYA WASANII "WASANII TUTAZIDI KUPUKUTIKA MAANA TUNAROGANA SANA..NATAMANI KUACHA MUZIKI ILI NIYANUSURU MAISHA YANGU"

0

 photo SHILOLE.jpg
MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kuwa, suala la wasanii wa muziki kurogana linamuumiza kichwa kiasi cha kufikiria kuachana na kazi hiyo.

Akiongea na mwandishi wetu pasipo kuwataja  wabaya  wake, Shilole alisema hivi sasa ‘kesi’ za wasanii kurogana zimeshika kasi kuliko siku za nyuma na anashindwa kuelewa ni kwa nini watu wanamuasi Mungu kwa kuendekeza ushirikina.

“Kwa staili hii wasanii tutazidi kupukutika, kuna wakati huwa nafikiria hata kuachana na muziki maana tunarogana na namuomba Mungu usiku na mchana hata kabla ya kupanda stejini kwani hali ni tete,”
alisema Shilole.

VANESSA MDEE- CLOSER OFFICIAL VIDEO

0

MAANDALIZI YA MSIBA MWANA HIP POP LANGA KILEO.

0

 
clip_image001
Hapa ndipo alipokuwa analelewa Langa kwa wazazi wake baba na mama na hizi picha ni wasanii wakifanyiwa mahojiano na waandishi wa habari kutoka Star TV na EATV. Picha ya juu ni Kalapina na picha za chini ni Kala Jeremiah

Ni Nyumban kwa Marehem Langa hapa Kalapna akmuongelea Mwana hiphop Mwenzie Marehem Langa,Pina amesema ameumia sana kwani Langa alkuwa Mwanahiphop aliekuwa akifata Misingi ya Hiphop.
RIP Langa

DIAMOND PLATNUMZ AAMUA KUWAPONDA BARAZA LA SANAA LA TAIFA BASATA

0

http://db2.stb.s-msn.com/i/7A/A7475481D3E98F4526A1F46ECAE19_h498_w598_m2_cOkykDiCU.jpg


Diamond Platnumz amelishukia Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA kuwa linaurudisha nyuma muziki wa Tanzania kutokana na kutoruhusu kuanzishwa kwa tuzo zingine za muziki nchini tofauti na Kilimanjaro Music Awards...

Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM leo, Diamond amesema hatua hiyo inamfanya ahisi kuna kitu kimejificha ndani ya baraza hilo.

“Kwanini Tanzania tuna tuzo moja, ni kitu ambacho kinanisikitisha sana kwasababu ukiangalia hata nchi zingine ni ndogo sisi tumewazidi kimuziki lakini zina tuzo zaidi ya moja,” alihoji Diamond.

“Sijui BASATA kuna nini kinaendelea.”

Amesema kungekuwepo na tuzo za aina mbalimbali za muziki nchini, kungekuwa na changamoto chanya kwa waandaji wa tuzo hizo kuliko hivi sasa ambapo KTMA haina mpinzani.

“Kukiwa na tuzo tofauti hawa watajifunza kupitia wale, lakini kitu kikiwa kimoja kila siku vinapelekwa tu.”

Kwa upande mwingine Diamond amesema baada ya nominations za Kili kutoka, hakuweza kuongea chochote kwakuwa aliona aliwekwa kwenye vipengele ambavyo hakustahili.

“Ukitazama kabisa kama sikuwa katika category yeyote naweza vipi kuwa msanii bora wa kiume, kwa kigezo kipi,” alihoji.

“Sasa unaniambia mimi sina sifa ya kuwa mbunge, diwani, waziri, sina sifa hizo halafu ukanishindanisha urais sasa ntashinda vipi kama huko mwanzo tu siwezi.”

“Nikaona you know what bora nipige zangu kimya sikutaka kuongea kwasababu hawachelewi kukutafsiri vingine, ndio maana sikuwepo siku zile, kiukweli kabisa.”

ORIJINO COMEDY: MKATABA MPYA WA ORIJINO KOMEDI NA KAMPUNI YA NEXUS

0

Kundi la Orijino Komedi linalotengeneza kipindi “Ze KOMEDI SHOW” kinachoongoza kwa kuangaliwa sana nchini limeingia mkataba na Kampuni ya Nexus Consulting Agency kwa kushirikiana na Rockstar4000.
Mkataba huo unaipa nafasi Orijino Komedi kuwa wasanii wa kwanza wa luninga kufanya kazi na Nexus.
Nexus Consulting Agency imenunua haki zote za usimamizi wa biashara na uongozi wa kundi la hilo la Komedi ambalo kwa miaka kadhaa sasa limekuwa namba moja katika sanaa ya uchekeshaji. Mkataba huu utakuwa kwa ajili ya kusimamia kipindi cha Orijino Komedi kuweza kuendelea kuwa namba 1 Tanzania na pia kupanua utazamwaji wake nje ya mipaka ya Tanzania.

Tour ya Washindi wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music awards 2013 yazinduliwa leo jijini Dar

0



Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Music Tour unaotarajiwa kuanza wiki ijayo Mkoani Dodoma,wakati wa mkutano uliofanyika leo katika Hoteli ya Holiday Inn jijini Dar es Salaam.Kulia ni Rais wa Bendi ya Mashujaam,Charles Baba na Muimbaji wa nyimbo za kizazi kipya, Diamod Platinam.




Mwimbaji wa nyimbo za nyimbo za kizazi kipya,Diamond Platinam (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Tour uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe na Rais wa Bendi ya Mashujaam,Charles Baba.




Mwimbaji wa nyimbo za kizazi kipya,Kala Jeremier (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Tour uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Wengine pichani toka kutoka kulia ni Rais wa Bendi ya Mashujaam,Charles Baba, Mwimbaji wa nyimbo za nyimbo za kizazi kipya,Diamond Platinam na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe.



Rais wa Bendi ya Mashujaam,Charles Baba(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Tour ulifanyika Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe na Mwimbaji wa nyimbo za nyimbo za kizazi kipya,Diamond Platinam.



Waimbaji na washindi wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro wakati wa uzinduzi wa Kili Muzic Tour uliofanyika leo katika Hotel ya Holiday Inn jijini Dar es Salaam.