ORIJINO COMEDY: MKATABA MPYA WA ORIJINO KOMEDI NA KAMPUNI YA NEXUS
0
Kundi la Orijino Komedi linalotengeneza kipindi “Ze KOMEDI SHOW” kinachoongoza kwa kuangaliwa sana nchini limeingia mkataba na Kampuni ya Nexus Consulting Agency kwa kushirikiana na Rockstar4000.
Mkataba huo unaipa nafasi Orijino Komedi kuwa wasanii wa kwanza wa luninga kufanya kazi na Nexus.
Nexus Consulting Agency imenunua haki zote za usimamizi wa biashara na uongozi wa kundi la hilo la Komedi ambalo kwa miaka kadhaa sasa limekuwa namba moja katika sanaa ya uchekeshaji. Mkataba huu utakuwa kwa ajili ya kusimamia kipindi cha Orijino Komedi kuweza kuendelea kuwa namba 1 Tanzania na pia kupanua utazamwaji wake nje ya mipaka ya Tanzania.