RAIS OBAMA KUFUNGA HOTELI YA NYOTA 5 KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM
0
Wakati Rais wa Marekani, Barrack Obama akitarajiwa
kuwasili na msafara wa watu 700, baadhi ya hoteli zenye
hadhi ya nyota tano jijini Dar es Salaam zimeanza
kusitisha kupokea wageni kutokana na ujio huo.
Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani ilisema
Rais huyo, anatarajiwa kuwasili nchini Julai Mosi kwa
ajili ya ziara ya siku tatu hadi Julai 3 mwaka huu ili
kuimarisha uhusiano baina ya nchi hiyo pamoja na nchi
za Afrika. Msafara huo utajumuisha watu mbalimbali
wakiwamo wafanyabiashara.