MAREKANI YAUNDA SHERIA KUWADHIBITI WANAUME WANAOVAA SURUALI CHINI YA MAKALIO YAO
0
Sina shaka umeshasikia style za uvaaji wa suruali
hususan kwa wanaume zenye majina kama mlegezo au kata k, au yawezekana ukawa
huzijui kwa majina lakini umeshashuhudia vijana wamevaa suruali chini ya
makalio.
Kama ambavyo mabinti wamekuwa wakilaumiwa kwa mavazi
ya kuonyesha miili yao hasa sehemu nyeti, na upande wa wanaume wamekuwa
wakilalamikiwa kwa style hiyo ya uvaaji ambayo imeonekana kuigwa hata na vijana
wadogo ambao bado wako shuleni.
Katika hali ya kukerwa na tabia ya vijana kuvaa
suruali chini ya makalio uongozi wa Wildwood, New Jersey nchini Marekani
umeandaa sheria mpya itakayoweza kuwadhibiti wale wote wenye tabia hiyo ya kuvaa
mlegezo na kukatiza mitaani.
Sheria hiyo inaelekeza wavaaji wote wa suruali,
kaptura, mavazi ya kuogelea na sketi zisivaliwe chini ya inchi 3 kutoka kiunoni
mwa mvaaji.
Mayor wa Wildwood Ernie Troiano Jr. aliwaambia
waandishi wa habari kuwa amechoshwa na malalamiko anayoyapata juu ya vijana
wanaotembea makalio nje kwa kushusha suruali zao kupita kiasi.
Unaonaje sheria kama hii ikija Tanzania
pia?