KHADIJA KOPA AFIWA NA MUMEWE
0
Mume wa Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki, Khadija Omar Kopa, aitwaye Jaffari Ally amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Marehemu alikuwa anasumbuliwa na matatizo katika mfumo wa upumuaji na mpaka mauti yanamfika alikuwa amelazwa katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN