ZIPOKEE HIZI PICHA 15 ZA MOJA YA MAJUMBA YA TAJIRI WA NIGERIA, NYUMBA INA MSIKITI NA KANISA NDANI.
0
Hili ni moja ya majumba ya kifahari yanayomilikiwa na Mnigeria anaeshika nafasi ya pili kwa utajiri Nigeria kwa mujibu wa jarida la Forbes Mike Adenuga, hili ni jumba la mabilioni ya Naira ambalo liko kwenye ardhi ya bei ghali inayomilikiwa na wachache wenye pesa Nigeria, panaitwa Banana Island.
Mike
Adenuga mfanyabiashara mkubwa Nigeria ambae pia ni mwenyekiti
wa Globacom, pamoja na utajiri alionao nimeona ripoti mbalimbali kwamba
amekua akitoa misaada ya mamilioni kwenye majanga tofautitofauti
Nigeria.
Ni jumba la kifahari ambalo pia lina msikiti na kanisa ndani yake ambapo kama haufahamu huyu ndio tajiri ambae aliwahi kuingia kwenye headlines Africa baada ya stori yake ya kumlipa Beyonce kuja kuimba kwenye harusi ya mtoto wake wa kike mwaka 2010.