ROMA MKATOLIKI AIACHIA NGOMA YAKE - 2030 MTANDAONI HII HAPA
habari mabibi na mabwana!! poleni na mihangaiko ya siku!! naam
ijumaa iliyopita nilitoa kibao changu maridhawa kipya kabisa kinaitwa 2030!!!
na nilikiachia kwa radio stations zote nchini kadri ya uwezo
wangu/wetu, though kutokana na mawasiliano ni ngumu kufikia radio
zote kwa wakati, ila nyingi ziliupata!!!
lakini niliweka utaratibu
fulani kwa watakaohitaji kuupata huo wimbo 2030 mbali na radio basi
wataupata kwa kussuport kuununua on line kwa tsh
3000/=!!nilishatangaza sana mnafahamu!!ilikuwa ni trial ya kuona nani
ana love ya kussuport na nani hana kupitia njia zilizowekwa na sio
njia nyingine.
zoezi limeenda kwa challenge nyingi sana asante
wote waliossuport katika hili, pia asante kwa wale
walioliharibu zoezi hili maana imenifanya nimtambue hu z real na hu z
fake!!!
imeniuma kuona wapo wasanii wanafanya biashara kama hii
wanauza mix tapes, album,tisherts zikiwa zote ni movements za kuleta
changes ktk mziki wetu, then hao hao wanakuwa mstari wa mbele kupinga
hii movement yangu halafu bila sababu yani dah SHALL WE MAKE IT?????
nway lilikuwa ni zoezi lililopangwa kufanyika kwa week moja 1 tu
ili kuona na kufanya tathmini kuwa yanawezekana haya?najua wengi
wanasubiri feed back ya mauzo haya haikuwa nzuri sana kwa wingi wa
nyomi nililokuwa nalo, lakini pia haikuwa mbaya maana ni mageni
haya..kwa siku 7 za mauzo ilikuwa kila siku wananunua watu
wasiopungua 50!! so unaweza ona hapo kuwa yanawezekana haya
tukiyawekea mkazo...ILA SIAMINI KAMA KILA MSANII ANAWEZA FANYA,
INATEGEMEA NA NGUVU YA MSANII HUSIKA NA KIBAO ALICHOKITOA..(IFIKIE
KIPINDI TUONGEE UKWELI TUU!!)wengi wameanza kufanya biashara kupitia
nyimbo hii na inawanufaisha wao, wengi wamerecord radio wimbo huu
kitu kilichopelekea kukosa quality na bado wanauzia wengine so
wanapewa kitu kisicho na quality, pia wengi wanakwazika na mengi
yaliyoongelewa ndani ya wimbo huu na wanakosa majibu maana wanakosa
fursa ya kuusikia mara kwa mara kwasababu hawajaunga mkono hii
movement!! au pengine imekuwa ni njia ngumu kwao kuupata,
basi kwa wale waliossuport kwa kuinunua nawashukuru sana na mungu
awaongezee mlipopungukiwa, najua litatokea hili la kujiona wanyonge
kuwa ROMA amechukua fedha zetu na kisha ameachia bure, mi naamini
ukiwa muelewa na ukiona nilichokisema hapo juu hautakwazika as long
umeonyesha lav yako kwa msanii unayemfeel, samahani sana kama nitakuwa
nimekukosea,nimefanya hivi kama kuanzisha hiki kitu na naamini
wengine watafatia na kukiboresha zaidi!!LAZIMA APOTEE MMOJA ILI
KUMI WAISHI VEMA NDIPO YATAPATIKANA MAENDELEO!! AM SO SORRY!!!
So leo wiki imetimia na wimbo umetoka rasmi na hauuzwi tena kama ilivyotangazwa awali.
unapatikana bure kwenye net, download via access yoyote
utakayoiona!! nimeutoa rasmi kwenye blogs mbali mbali ANZIA NA YA DJ
CHOKA, na nyinginezo!!
Na version iliyopita kuchezwa radio ni
version ya ROMA ile beat yake iliyochangamka ambayo ni version ya 1
ambayo ndiyo ilikuwa ya kwanza kutambulishwa ijumaa pale clouds fm
radio.
kwa maswali zaidi tutameet kwenye mainterviewz huko maradioni na tutawekana sawa!!
samahanini kwa wote niliowakwaza, asanteni kwa wote mliossuport!! ROMA 2030 INAPATIKANA FREE SASA!!!