KAULI YA JESHI LA POLISI KUHUSU TAARIFA ZA AWALI ZA MAUAJI YA WATU KWENYE SHOW YA BARNABA FEKI KARATU.
0
Jeshi la Polisi Arusha limekanusha taarifa zilizoenea toka jana kwamba watu wanne walifariki October 21 2012 baada ya fujo kutokea kwenye Pub Lamonte Karatu ambayo ilitangaza kwamba Barnaba angeimba lakini baadae mashabiki wakagundua waliibiwa viingilio kwa sababu hakua Barnaba orijino.
Taarifa nilizozipata usiku huo kutoka kwa mwandishi wa habari wa Mlimani Tv ziliamplfy kwamba mauaji hayo yalitokana na ugomvi wa chupa na visu.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha amesema hakuna mauaji yoyote yaliyotokea usiku huona kwamba amepigiwa simu nyingi sana na waandishi wa habari wakiulizia hizo taarifa.
Mmoja kati ya watu walioshuhudia ambae pia alilipa kiingilio kumuona Barnaba amesema kweli fujo zilitokea na watu walimpiga chupa yule Barnaba feki baada ya kumgundua ni muongo na alikua hawezi kuimba nyimbo za Barnaba kwenye stage, alikua anajikanyaga kanyaga kabla ya kuokolewa na mabaunsa kwa kutolewa kwenye hiyo pub.
Shahidi huyu aitwae Ibrahim amesema ukumbi ulikua na watu wasiopungua 200 na mpaka sasa hawajarudishiwa viingilio vyao na wala mmiliki hana time nao na wala hajapatikana uizungumzia hii ishu.
Kwa mujibu wa Ibrahim, hii ni mara ya pili kwa Pub hiyo kupeleka msanii feki… wa kwanza alikua Ally Kiba ambae watu waligundua wameibiwa lakini hawakufanya chochote, millardayo.com bado inamtafuta mmiliki wa hiyo Pub ili kupata stori kamili.