Dr. Aleck Che-Mponda na wenzie walivyopambana na ubaguzi wa rangi marekani miaka ya 1961
0
Na Cheni Che-MpondaWadau, leo hii mtu wa rangi yeyote akija Marekani, anaweza kula sehemu yoyote, kwenda shopping sehemu yoyote na kuishi sehemu yoyote anayotaka bila kujali rangi. Ni hela yako tu. Lakini si miaka mingi uliyopita maisha hayakuwa hivyo kwa watu weusi. Weusi walibaguliwa Marekani kutokana na historia ya Utumwa. Ingawa utumwa ulifutwa mwaka 1865, ubaguzi dhidi ya weusi uliendelea. Ulipungua baada ya Civil Rights Acts (14th Amendment) ya mwaka 1964.Miaka ya 1950's mwishoni na 1960's nchi za Afrika zilianza kupata Uhuru.