BONGO FLAVA - NURAH NAE ASEMA

0



Msanii mkongwe wa Bongo Flava, maarufu kama Nurah ametoa maoni yake katika swala zima la muziki wa bongo flava, akiongea kama Interllectual Nurah amesema "mimi kama mimi naamini haki za wasanii zipo, tena zipo kabisa. Tatizo ni kwamba wasanii wengi haatuzifahamu na hatujui nani anajukumu la kuhakikisha haki zetu zinafuatwa. Mimi nikipata tatizo leo sijui nimfate nani, BASATA au COSOTA, labda la kushauri ni sisi wasanii wenyewe tuwe na umoja na tufatilie ni wapi tunaweza kuzipata haki zetu kwasababu mimi mwenyewe naamini kuna haki zangu nyingi sana ambazo bado sizijui" alisema Nurah
Pia Nurah alipoulizwa kwa baadhi ya wasanii kujitoa katika mashindano mbali mbali alisema "mimi naamini kwamba TID ni msanii ambae ana akili nzuri na ni mchambuzi, kama ameona Kili music awards haina faida kwake basi sio mbaya kama akijitoa".
Kwa sasa Nurah anamalizia mwaka wa mwisho katika chuo cha usimamizi wa fedha akijukua stashahada ya juu katika teknolojia ya habari na mawasiliano, "hii ndio sababu inayonifanya niwe kimya sana katika gemu" alimaliza msanii huyo maarufu kama Baba stlyz

0 comments: